19 Desemba 2025 - 19:07
Wafanyakazi 741 wa sekta ya afya wameuawa au kujeruhiwa wakati wa vita vya Sudan

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umetangaza kuwa tangu kuanza kwa vita nchini humo kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) mnamo Aprili 2023, jumla ya wafanyakazi 234 wa afya wameuawa na 507 wengine wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Katika kuendelea kwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya mwitikio wa haraka, vyanzo vya ndani na mashuhuda wa macho wameripoti kuwa droni kadhaa zililenga kituo cha kuzalisha umeme cha Al-Muqran katika mji wa Atbara, uliopo katika jimbo la Nile River kaskazini mwa Sudan. Shambulizi hilo limesababisha kukatikakatika kwa umeme katika miji mikubwa, ikiwemo Khartoum, Port Sudan, na majimbo mengine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya mkoa wa Nile, shambulizi hilo lilipelekea kuuawa kwa wafanyakazi wawili wa ulinzi wa raia, ambao walikuwa wakijaribu kuzima moto uliozuka baada ya shambulizi la kwanza la anga.

Chanzo cha kijeshi cha Sudan kimesema kuwa shambulizi hilo la droni lililofanywa na Vikosi vya Mwitikio wa Haraka pia lililenga njia kuu za usambazaji wa umeme katika miji ya Atbara na Ad-Damer, na kusababisha kukatika kwa umeme katika miji kadhaa ikiwemo Shendi.

Katika muktadha huo, Mtandao wa Madaktari wa Sudan umethibitisha kuwa tangu kuanza kwa vita mnamo Aprili 2023, umesajili vifo vya wafanyakazi 234 wa sekta ya afya na majeraha ya wafanyakazi wengine 507.

Taasisii hiyo pia imeeleza kuwa hatima ya wafanyakazi zaidi ya 59 wa afya bado haijulikani, huku wafanyakazi wengine 73 wakizuiliwa katika mji wa Nyala.

Kwa upande mwingine, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa zaidi ya raia 1,000 waliuawa mwezi Aprili uliopita, wakati Vikosi vya Mwitikio wa Haraka vilipodhibiti kambi moja katika eneo la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Tukio hili linaonesha kwa wazi athari kubwa za kibinadamu za vita, hususan kwa wahudumu wa afya ambao kwa mujibu wa sheria za kimataifa wanapaswa kulindwa wakati wa migogoro ya kivita.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha